VOLUME 3, ISSUE 2

Title: Kanuni za Utokeaji wa Viambishi vya O-Rejeshi katika Lugha ya Kiswahili


Authors: Phides Kagwa

 Phides Kagwa Idara ya Sanaa na Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu Teofilo Kisanji, S.L.P 1104, Mbeya, Tanzania.
 
*Correspondence: phideskagwa@yahoo.com,   Simu: +255 (0) 748 887 532


Ikisiri


Makala haya yanahusu kanuni za utokeaji wa viambishi vya O-rejeshi katika lugha ya Kiswahili hususan katika vitenzi na umbo la AMBA-. Mada hii itaongozwa na nadharia ya mashartizuizi katika mpangilio wa viambishi iliyoasisiwa na Bybee (1985) anasisitiza kuwa mpangilio wa viambishi huwa na uhusiano sawia, baina ya kiambishi kimoja na kingine. Pia, utokeaji wa viambishi hivyo huweza kutawaliwa na kanuni fulani, yaani viambishi hivyo havitokei kiholela hole bali hufuata kaida zinazotawala katika lugha husika. Hivyo, kuwepo kwa kiambishi {a} katika kitenzi husababisha kuwepo kwa kiambishi {b} katika kitenzi hicho. Wapo wataalamu mbalimbali wamejaribu kugusia suala la viambishi vya O-rejeshi katika lugha ya Kiswahili. Wataalamu hawa katika kutoa hoja zao kwa namna moja ama nyingine wamekinzana katika mazingira ya utokeaji wa viambishi hivyo kama ilivyojadiliwa na Kagwa (2021). Pia, hawakuweza kutoa kanuni zinazotalawa katika mazingira ya utokeaji wa viambishi vya O-rejeshi. Hivyo, Makala haya yataangazia kanuni zinazotawala mazingira ya utokeaji wa viambishi vya O-rejeshi katika vitenzi vya lugha ya Kiswahili huku tukiongozwa na nadharia ya Mashartizuizi.

Maneno ya Msingi: Viambishi vya O-rejeshi, Mazingira ya Utokeaji, kanuni,Vitenzi vya Kiswahili, kabla na mzizi na baada ya mzizi neno.

Download the Article